Msanii chipukizi wa bongo fleva, Bumbuli ambaye kwa sasa anatamba na singo yake inayokwenda kwa jina la ‘Kikwazo’, ametoa mpya iliyowashangaza watu baada kuagiza ugali dagaa ndani ya ndege.

Msanii huyo ikiwa ni mara yake ya kwanza kupanda ndege amefanya kioja hicho, tukio lililofanya wasanii wenzake kuangua kicheko. Kioja hiko kilitokea pindi wanatoka mkoani Mwanza kurudi Dar es salaam, baada ya kufanya shoo.

Bumbuli amemtupia lawama hizo Muheshimiwa Temba ambaye anadai kuwa ndiye aliyemlaghai na kumwambia waagize ugali dagaa ili wale, na kwake ilikuwa rahisi kuamini uwepo wa ugali dagaa ndani ya ndege kwani aliona wenzake wakinywa na kula vyakula mbalimbali, pia ukizingatia ilikua mara yake ya kwanza kupanda ndege.

Amesema Bumbulu ”Unajua nini, ni mara yangu ya kwanza kupanda ndege, sasa Muheshimiwa Temba akaniambia nimuite muhudumu yule niagizie ugali na dagaa tule wote. Kwa kuwa niliona watu ndani ya ndege wanakunywa vinywaji mbalimbali niliamini kuwa kweli kuna ugali, nikamuita, nikaagiza. Nikashangaa kusikia kia mtu anacheka,”.

 

 

?Live: Rais Magufuli akizindua rasmi maonyesho ya Sabasaba
Video: Vimbwanga vyatawala ulipaji kodi ya majengo, Spika awalipua wapinzani bungeni