Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Meja Jenerali Gabriel Mhidze amesema MSD iko mbioni kuanzisha kiwanda cha dawa za ngozi,ikiwemo mafuta maalumu ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Meja Jenerali Mhidze amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa tayari mashine za kiwanda hicho zimeshafika kitazalisha pia dawa za meno na dawa za macho.

“Wakati naingia hapa MSD Mei mwaka jana, hali ilikuwa siyo nzuri, kwani tuliingia wakati wa janga la Covid – 19, barakoa ilikuwa ikiuzwa kwa bei ya juu, vitakasa mikoni navyo hali ilikuwa hivyo hivyo” amesema Meja Jenerali Gabriel

Mabalozi wapangiwa vituo

“Hata usambazaji wa dawa nao haukuwa mzuri, na sababu kubwa niliambiwa ni kutokana na Corona, niliwaita wataalamu tulionao hapa MSD  na tukakusanya mawazo kupitia maandiko, kisha tukawawezesha (wataalamu) ili waanze kutekeleza,” amesema Meja Jenerali Gabriel

Aidha amesema kuwa kiwanda cha  MSD cha kuzalisha mipira ya mikono kilichopo imIdofi, Makambako mkoani Njombe kinatarajiwa kuanza uzalishaji mwezi Novemba mwishoni,huku akisema viwanda vingine vya dawa za rangi mbili, vidonge na dawa za maji maji za watoto mashine zake zimeshaanza kuwasili.

Tayari ina viwanda vya kuzalisha barakoa na dawa Keko jijini Dar es Salaam,ambavyo vinauwezo wa kuzalisha aina 10 za dawa na barakoa.

Manny Pacquiao ajiweka pembeni
Diara afichua siri ya ubora wake