Baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kuonesha kuwa kuna vifaa vya shilingi bilioni 2 ambavyo vinaonekana vinasafirishwa kutoka Bohari la ya Dawa (MSD) iliyoko maeneo ya Keko Dar es Salaam kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) iliyoko Upanga jijini humo, Uongozi wa MSD umepinga taarifa hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu  jana amesema kuwa Bohari hiyo haina mzigo wowote ulio njiani kuelekea Muhimbili na kwamba taarifa zinazoonesha hivyo zilitokana na tatizo la kuhamishwa kwa mfumo wa kompyuta uliokuwa unatumika mwaka 2012.

“Mwaka 2012 tulibadilisha mfumo wa kompyuta kutoka wa awali mpaka tunaotumia sasa, hivyo kuna miamala ilihitaji kubadilishwa, mwaka huu tulifanya zoezi la kukamilisha baadhi na si kwa Muhimbili pekee kwa mfano kuna mzigo unatoka MSD Ubungo kwenda Muleba ukifika kule mtu anashindwa kuingiza kwenye mfumo kwamba umepokelewa,” alisema Bwanakunu.

Bwanakunu aliongeza kuwa tayari walitoa majibu yao kwa CAG na kumueleza kuwa walitengeneza timu ya uchunguzi na kwamba kuna baadhi ya watumishi walishawajibishwa huku akisisitiza kuwa hakuna mzigo uliopotea.

Wakati Bwanakunu akieleza hayo waandishi wa habari, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewaitaka Bohari hiyo kumpa maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu sakata hilo.

Boban, Temi Nje City Ikiivaa Mtibwa J’mosi
TFF Yatangaza Muelekeo Wa katiba Ya Yanga