Kauli ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kupitia kitabu chake cha “My life My Purpose” imeungwa mkono na Spika mstaafu waa bunge la Tanzania Pius Msekwa  kuwa baadhi ya wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi mkuu 1995 walikua na hoja dhaifu na kupelekesa rais mstaafu Mkapa kupata.

Ametoa maoni yake juu ya juu ya kitabu kilchozinduliwa hivi karibuni, ambapo mambo yaliyoelezwa kwenye kitabu hicho kuhusiana na uchaguzi mkuu wa 1995 ni kwamba wapinzani wake walikuwa wadhaifu wa hoja.

Pius Msekwa amesema kuwa “Kiukweli hata mimi ninachokikumbuka ndiyo kile ambacho amekisema Mkapa, ila yeye amepata muda zaidi wa kuangalia mambo aliyokutana nayo, niwasihi tu vijana kasomeni yale ya kwenye Kitabu na myazingatie kabisa.”

Novemba 12, 2019 ikiwa siku yake ya kuzaliwa Rais Mstaafu Mkapa, kilizinduliwa kitabu chake alichokiita kwa jina la ‘My Life, My Purpose’, ambapo viongozi mbalimbali wa Kitaifa walishiriki, akiwemo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na  marais wastaafu, Jakaya Kikwete pamoja Ali Hassan Mwinyi.

Undani wa Picha ya mtoto akichungulia darasani na sufuria mkononi
Wanawake wakiislamu Kagera waomba msaada ujenzi wa Hospitali ya mama na watoto