Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, amesema kwa sasa Serikali haioni cha kujibu juu ya waraka uliotolewa na Baraza la maaskofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri nchini Tanzania, (KKKT).

Amezungumza hayo pindi alipohojiwa juu ya waraka huo uliotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibua baadhi ya mambo ambayo yalitajwa kuwa ndio tishio kubwa la umoja na amani nchini.

Ambapo mambo yaliyotajwa katika waraka huo ni pamoja na utekwaji wa watu, utesaji, kupotea kwa watu, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.

Aidha Dk. Msemaji huyo wa Serikali amesema kuwa kwa sasa hana la kusema zaidi tu inawatakia waumini kheri ya pasaka.

 

Miguna aendelea kuzuiliwa uwanja wa ndege Nairobi
Kitenge chatakiwa kuwa vazi rasmi Afrika Mashariki badala ya suti