Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa Rais Dkt. John Magufuli hajakataa kutekeleza ongezeko la mshahara la mwaka la watumishi wa umma na kuwataka TUCTA kuacha siasa.

Ameyasema hayo hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa hoja ya Rais Magufuli kutokuwaongezea mishahara watumishi wa Umma ilizushwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusema Rais Magufuli hakusema jambo hilo.

“Hakuna mahali Rais Magufuli alipokataa kutekeleza ahadi ya ongezeko la mwaka la mishahara ya watumishi wa umma, Serikali imetenga Bil. 487.7 kuwalipa wafanyakazi wanaopanda madaraja kwa mwaka huu wa fedha,”amesema Dkt. Abbas

 

Kamusoko kukaa nje ya dimba kwa wiki mbili
Video: Chris Brown aachia ngoma mpya yenye masharti kuitazama

Comments

comments