Mshambuliaji wa Coastal Union Maabad Maulid Maabad, amewaomba radhi wadau wa Soka la Bongo kwa tukio la utovu wa nidhamu alilolionyesha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC.

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex-Chamazi Jumapili (Novemba 27), ulishuhudia Coastal Union ikipoteza kwa mabao 3-2, bao la tatu la wenyeji lifungwa dakika za lala salama na Kiungo Mshambuliaji Iddy Seleman ‘Iddinado’.

Maabadi alionekana akirushwa Chupa za Maji na Kiatu kwa nyakati tofauti kumlenga Mwamuzi wa mchezo huo, ambao ulichezwa kwa dakika 101, baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika na kuongezwa nyingine nne ambazo hazikuchezwa kutokana na Mlinda Lango wa Coastal Union Mohamed Mroivili kutumia dakika kadhaa kulalamika alikuwa na maumivu.

Maabad amesema mwili wake ulikuwa umepata joto kutokana na mchezo wenyewe kuwa mgumu, hivyo alijikuta anaingia kwenye changamoto ya kuona maamuzi yaliokuwa yanafanyika dhidi yao hayakuwa na haki na kuamua kuchukua uamuzi wa Jazba.

“Kwa mujibu wa sheria 17 za mpira wa miguu naomba radhi kwa wadau wote na wachezaji wenzangu.” amesema Maabadi

Wachezaji Young Africans wapigwa marufuku

Hata hivyo Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi, inatarajiwa kutoa maamuzi kuhusu tukio hilo baada ya kupitia ripoti za mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Coastal Union, sambamba na Michezo mingine ya Ligi Kuu iliyochezwa siku za karibuni.

Moses Phiri: Naweza kuwa mfungaji bora
Juma Mgunda: Tuna kazi kubwa Tanga