Raia wa Marekani wamejitokeza kwa wengi kuelezea kusikitishwa kwao na shambulizi la halaiki katika klabu ya mashoga mjini Orlando huku wakisema kuwa sera legevu za kudhibiti umiliki wa bunduki nchini humo zimechangia kuongezeka kwa visa vya aina hiyo.

Kulingana na taarifa za polisi, mshambuliaji huyo kwa jina Omar Mateen alivamia klabu hiyo karibu saa nane usiku akiwa amejihami na bunduki mbili na kuua watu 50 huku akijeruhi wengine 53 kabla ya kupigwa risasi na kuuawa na polisi baadaye.

Duka-BindukiMatee, 29, ambaye ni raia wa Marekani mwenye asili ya Afghanistan anasemekana kununua silaha hizo kihalali kutoka kwa duka inayouza bunduki licha ya kuwa wakati mmoja alichunguzwa kwa kuwa na itikadi kali. Wengi wanajiuliza kwa nini serikali ingali inaruhusu watu wenye itikadi kali kama Mateen kupata silaha hatari.

Video: Naibu Waziri Abdallah Possi ameitaja mikakati kuondoa unyanyapaa kwa watu wenye Ualbino
Viongozi wa mfuko wa Pamba wameumbuliwa