Mtu mmoja aliyekuwa na silaha (Bunduki), amewashambulia na kuwauwa watu sita kwenye duka kubwa la Walmart lililopo jimbo la Virginia nchini Marekani, likiwa shambulizi la pili lililouwa watu wengi nchini humo katika muda wa siku chache.

Kwa mujibu wa shahidi mmoja, amesema wakati wa shambulizi wateja walikuwa wamefurika dukani kununua bidhaa mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya kutoa shukrani.

Mashuhuda wakijadili jambo jirani na eneo la tukio. Picha ya The New York Times.

Hata hivyo, mshambuliaji aliuawa katika mkasa huo, ingawa Polisi wamesema hawakuhusika katika kifo chake licha ya watu kudai ilitakiwa iwe hivyo ili kuepusha madhara zaidi.

Kwa mwaka huu pekee, Marekani imekuwa na visa 40 vya mauaji ya watu wengi kwa kutumia bunduki, ukiwa miongoni mwa miaka iliyosajili visa vingi vya matukio hayo.

CAF yataja tarehe mpya Makundi Afrika
Juma Mgunda: Haiwi mwisho hadi ifike mwisho