Ikiwa imebaki siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar (Machi 20), Jeshi la Polisi visiwani humo limemshikilia Mansoor Yusuf Himid, mshauri wa Katibu Mkuu wa Katibu Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.

Mwanasiasa huyo alishikiliwa jana na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano muda mfupi baada ya Jeshi hilo kumpigia simu.

Akiongea na BBC mapema leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kuwa jeshi hilo limewashikilia Mansoor pamoja Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Hamad Masoud kwa mahojiano kuhusu milipuko ya mabomu katika maskani ya CCM, Kisonge mjini Magharibi pamoja na bomu lililolipua nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi visiwani humo.

Alisema Jeshi hilo pia linawashikilia viongozi hao wa CUF kutokana na kauli zao walizozitoa na zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi pia linawashikilia watu wengine 42 kutokana na matukio hayo na limeendelea kuwahakikishia wananchi kuwa hali ni shwari na wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi wa marudio.

“tunataka maelezo na tukishapata maelezo yake tutaamua kama ni kumwachia au la, lakini kwa sasa tunamhitaji kwa kuisaidia polisi kwenye upelelezi,” alisema Kamanda Mkadam.

Wakati hayo yakiendelea, Jana Maalim Seif alikazia msimamo wa chama chake kutoshiriki uchaguzi wa marudio visiwani humo.

 

 

Sports Club Villa Hawakufanya Mazoezi Aman Stadium
Liverpool Wasubiri Droo Ya Robo Fainali Europa League