Ni moja kati ya mashindano makubwa zaidi ya michezo mbalimbali duniani ikianzishwa miaka ya nyuma kabla ya kristo na michuano ya kwanza kufanyika huko nchini Ugiriki, ambayo kwa mwaka huu ikifanyika katika mji mkuu wa nchini Brazil huko Rio De Janeiro ikipewa jina la ‘Rio 2016’

Mpaka sasa michezo hiyo imekwishafanyika kwa kiwango kikubwa na hivyo kupata Orodha ya timu zinazoongoza mpaka sasa katika kunyakuwa medali nyingi kwa upande wa Dhahabu, Shaba pamoja na Fedha huku jumla ya mataifa 206 yanashiriki Olimpiki ya mwaka huu.

Marekani ni nchi kinara katika medali hizo, huku ikiwa na jumla ya medali 27 kwa kujumuisha michezo yote na mpaka kufikia leo, akijinyakulia medali 10 za dhahabu, 8 za shaba pamoja na medali 9 za Fedha.

Nchi inayofuatia ni China wakiwa na medali 17 mpaka sasa wakiwa na medali 8 za dhahabu medali 3 za shaba pamoja na medali 6 za fedha, kwa hiyo China kuwa nchi ya kwanza kwa kuwa na medali nyingi za Dhahabu akifuatiwa na Marekani ikifuatiwa na Australia.

Nchi zingine ni pamoja na Australia mwenye medali 8 mpaka sasa huku akiwa na medali 4 za dhahabu 4 za Fedha na kuambulia patupu katika medali ya Shaba.

Kiujumla katika medali zote Urusi imeshikilia nafasi ya nne kwa jumla ya medali 12, Japani 12 huku ikifuatiwa na Italia medali 9, Korea Kusini medali 6 pamoja na Ufaransa 6, Canad 5, huku Hungary pamoja na Thailand zikiwa na medali 4.

Ujerumani pamoja na Taipei ya China zote zina medali 3, huku wenyeji Brazil, Ubelgiji, Ugiriki, Uholanzi, Sweden zote zikiwa na medali mbli kila moja, na nchi pekee kutoka Afrika, Afrika Kusini ikiwa na jumla ya medali mbili amabzo zote ni za Fedha moja ikipatikana katika kuogelea walizoshinda Cameron Van De Burgh pamoja na Chad Le Clos.

Ratiba Ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara 2016/17 Yapanguliwa
Azam FC Kucheza Mchezo Wa Kimataifa Wa Kirafiki