Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 24 za makundi A, B, C na D kucheza katika viwanja 12 mbalimbali nchini, kusaka nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao (StarTime First League).

Kesho Jumamosi Kundi A, Singida United watakua wenyeji wa Mvuvuma FC katika uwanja wa Namfua mkoani Singida, Green Warriors watacheza dhidi ya Mirambo FC uwanja wa Mabatini Mlandizi – Pwani, huku maafande wa Trasnit Camp wakiwakaribisha Abajalo FC ya Tabora katika uwanja Kambarage Shinyanga.

Kundi B, jijini Mwanza timu ya Alliance FC itawakaribisha ndugu zao Pamba FC katika uwanja wa CCM Kirumba, Madini FC ya mkoani Arusha ikiwakaribisha Bulyanhulu FC uwanja wa Mbulu, huku AFC wakicheza dhidi ya JKT Rwamkoma katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kundi C, Abajalo FC ya jijini Dar es salaam watawakaribisha Changanyikeni FC katika uwanja wa Karume, huku kundi D, Mbeya Warriors watakua wenyeji wa Wenda FC uwanja wa Sokoine – Mbeya, Sabasaba FC dhidi ya Mkamba Rangers uwanja wa Jamhuri Morogoro, na The Mighty Elephant watakuwa wakicheza dhidi ya African Wanderes kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Jumapili kutakua na mchezo mmoja kati ya  Vill Squad dhidi ya Karikaoo ya Lindi kwenye uwanja wa Karume, Jumatatu Cosmopolitan FC watawakaribisha Mshikamano FC katika uwanja wa Karume yote ikiwa michezo ya Kundi C.

Ujerumani yammwagia Sifa Magufuli
Point Tatu Za EPL Kusakwa Weekend Hii