Kampuni moja ya shughuli za mazishi nchini Italia, inamtafuta kwa bidii mtu mmoja ambaye alishinda bahati nasibu ya kupewa huduma za kuzikwa bure.

Hatua hiyo, inakuja baada ya mtu huyo kushindwa kujitokeza na kudai zawadi yake kwa muda wa miezi saba sasa, ambapo mchezo huo wa bahati nasibu uliisha kwa mtu aliyepeta tiketi ya namba 11 kuibuka mshindi.

Zawadi ambazo anatakiwa kupewa mshindi huyo ni jeneza, eneo la kuzikwa, vinara vya mishumaa, kuchimbiwa kaburi bure na kuendeshewa shughuli zote za sala kwa malipo ya kampuni hiyo.

Hata hivyo, pamoja na matangazo mbalimbali mshindi huyo hajajitokeza hadharani ili ahakikishiwe zawadi zake ambazo atazitumia muda wake ukifika na Kampuni kaikutaja tarehe ya mwisho ya kudai zawadi hizo.

Polisi Tanzania yaitumia salamu Simba SC
Leonardo Bonuchi atangaza kustaafu soka