Takriban saa nne na nusu usiku Afrika Mashariki, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo au Neymar Jr atatangazwa kuwa mshindi wa Ballon d’Or, tuzo anayopewa mchezaji bora zaidi duniani. Mshindi hupatikana kutokana na kura zinazopigwa na makocha wa timu za taifa, manahodha na waandishi wa habari. Hii ni mara ya 60 kwa tuzo hii kutolewa, katika hafla itakayofanyika jijini Zurich, Uswisi.

Kipindi cha uwezo wa wachezaji hawa kimetazamwa kuanzia Novemba 22, 2014, hadi Novemba 20, 2015. Upigaji kura ulianza Oktoba 26, 2015 na kumalizika Novemba 20, 2015.

Kutakuwa na tuzo kadhaa zitakazotolewa pia katika hafla hiyo. Tuzo ya Fifa Puskas (goli bora la mwaka), tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka, meneja bora wa mwaka, na timu bora ya mwaka FIFpro kutajwa.

Tuzo ya mchezaji bora wa kike: Carli Lloyd (Marekani), Aya Miyama (Japan), na Celia Sasic (Ujerumani)

Kocha bora wa mwaka: Luis Enrique (Barcelona), Pep Guardiola (Bayern Munich), na Jorge Sampaoli (timu ya taifa ya Chile)

Je Cristiano Ronaldo ataweza kushinda kwa mara ya tatu mfululizo na kumfikia Messi kwa kushinda tuzo kwa mara ya nne? au Messi atanyakua kwa mara ya tano na kuweka rekodi? au Neymar atanyakua tuzo yake ya kwanza?

Elimu Bure Yaanza Rasmi, Msako Wa wanaowapa Mimba Wanafunzi Waanza
Watumiaji wa iPhone wacharuka, Wasaini Kupinga ujio wa iPhone 7 Hii