Idara ya Polisi ya Los Angeles, imesema mesitisha juhudi za kumtafuta mtu huyo aliyejihami kwa bunduki na kuwauwa watu 10 huko California, katika sherehe za kuadhimisha Mwaka Mpya wa Lunar baada ya kuupata mwili wake ukiwa katika gari.

Mkuu wa Polisi wa Los Angeles, Robert Luna amesema wameupata mwili huo ukiwa na jeraha la risasi huku akifafanua kuwa, “Mshukiwa ametambuliwa kama Huu Can Tran (72), mwenye asilia ya Asia. Ninathibitisha kwamba hakuna washukiwa wengine kutokana na tukio hilo la mauaji katika uwanja wa Monterey.”

Polisi wakiwa katika eneo tukio Monterey Park, Calif jana Jumapili Januari 22, 2023 ambapo ufyatuaji risasi ulitokea baada ya sherehe ya Mwaka mpya kukamilika huko Los Angeles. Picha ya Jae C. Hong / AP.

Amesema, watu saba kati ya watu kumi waliojeruhiwa bado wako hospitali na tukio hilo lililofanyika katika mji wa Moterey Park, eneo lenye idadi kubwa ya Wamarekani wenye asili ya Asia, lilitilia kiwingu sherehe hizo ambazo kwa kawaida zinaadhimishwa China, Vietnam na Korea Kusini na kuitia hofu jamii hiyo.

Mauaji hayo, ni ya tano na makubwa kufanyika nchini Marekani mwezi huu na ni mabaya zaidi kufanyika tangu Mei 24 mwaka jana (2022), ambapo watu 21 waliuwawa katika shule moja huko Uvalde jimboni Texas huku Rais Joe Biden na Mkuu wa Sheria Merrick Garland wakiagiza mamlaka za shirikisho kusaidia katika uchunguzi wa tukio hilo.

Mpango ataka juhudi ushughulikiaji rushwa kwenye vyombo vya haki
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 23, 2023