Katika hali ya kusikitisha, msichana mmoja mwenye umri wa kati ya miaka 13 na 15 ambaye alibainika kuwa alibakwa na baba yake mzazi ameambulia kupigwa bakora na wanakijiji.

Washington Post limeripoti tukio hilo lilitokea katika kijiji cha panchayat nchini India na kuwekwa kwenye kipande cha video kilichosambazwa kupitia mitandao ya kijamii, ambapo wanakijiji kadhaa wanaonekana wakimnyooshea vidole na kumsonga msichana huyo ambaye amefungwa kiunoni.

Kosa lake lilitajwa kuwa kuogopa kutoa taarifa kuwa baba yake alikuwa anambaka kwa kipindi kirefu.

Msichana huyo aliyevaa nguo ya kaki aliambulia kuchapwa zaidi ya bakora 10 kabla baadhi ya wanakijiji wenye huruma kutaka ahurumiwe na kuondolewa adhabu hiyo.

“Inatosha… inatosha,” inasikika sauti ya baadhi ya wanakijiji inayomfanya mtoa adhabu aweke chini bakora yake.

Gazeti hilo lilifuatilia historia ya maisha ya msichana huyo na kubaini kuwa alikuwa anaishi na baba yake na hakuwahi kwenda shule. Alikuwa anajishughulisha na kazi mbalimbali za kumsaidia baba yake huyo ili kujipatia kipato na waweze kuishi.

India ni nchi yenye watu bilioni 1.2 na uchumi unaokuwa kwa kasi, lakini ni nchi inayoongozwa kwa matukio ya ubakaji pamoja na kujiua.

Fainali Ya Kombe La Shirikisho Yapelekwa Juni 11
Tani 622.4 za sukari zakamatwa mkoani Morogoro

Comments

comments