Katika hali ya kushangaza, msichana mwenye umri wa miaka 9 (mtoto) aliyeokolewa kutoka mikononi mwa wanamgambo wa Boko Haram katika msitu wa Sambisa nchini Nigeria, amegoma kula akitaka arudishwe akaishi na mumewe ambaye ni mgambo wa Boko Haram.

Msichana huyo ambaye jina lake halikutajwa ni miongoni mwa wasichana 65 waliokolewa hivi karibuni kutoka kwenye msitu huo. Kati yao, wengine wamekutwa wakiwa wajawazito na wengine wakiwa na watoto wachanga.

Kwa mujibu wa Vanguard, kisa hicho kilibainika baada ya Gavana wa Jimbo la Bono, Kashim Shettima alipoenda kutembelea kambi waliyowekwa wasichana hao hivi karibuni.

Ilibainika pia kuwa kati ya waliokolewa, watoto walikuwa 27 na zaidi ya wasichana wadogo 30 wakiwemowe wawili kutoka nchini Cameroon. Lakini wengi kati yao walikuwa tayari wamekolezwa kisaikolojia na kiimani kwakuwa walikuwa tayari kurudi tena msituni ili wakaishi na waume zao.

Picha: Utapenda alichofanya huyu mzee kwenye show kubwa ya Beyonce 'iliyomboa'
Afisa wa Jeshi la Uingereza ajiunga na magaidi wa ISIS, ana mafunzo ya hali ya juu

Comments

comments