Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu ameagiza kupelekwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili akatoe ushahidi wake wa namna ufisadi ulivyofanyika kwenye mradi wa mfumo wa uhamiaji mtandao (E-Immigration).

Ameyasema hayo baada ya Msigwa kudai kuwa ana taarifa za kutosha juu ya ufisadi uliofanyika katika mradi uliozinduliwa na Rais Dkt. Magufuli hivi karibuni na kudai kuwa Kambi ya Upinzani bungeni wanazo nyaraka za kutosha ambazo hazina mashaka kuhusu namna ufisadi ulivyofanyika katika mradi huo chini ya Serikali ambayo inajipambanua kupambana na ufisadi.

“Mhe. Msigwa taarifa ulizonazo kuhusu ufisadi uliofanyika kwenye hili zoezi zipelekwe kwenye hii kamati, Kamati itakuja kulishauri bunge tufanye nini na huo ufisadi unaoendelea hayo maeneo kwa hiyo naiagiza kamati imuite Mhe. Peter Msigwa na yeye namuagiza Mhe. Msigwa apeleke huko hizo nyaraka ili bunge liweze kushauriwa na kuchukua hatua mahususi,”amesema Dkt. Tulia

Hata hivyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  Januari 31, 2018  alizindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

 

Dalali: Hii ndio Simba ya siku zote
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 10, 2018