Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, amekanusha habari inayodai kuwa Rais John Pombe Magufuli ameshinda tuzo ya ”The African Prestigious Awards 2017” zilizotolewa nchini Ghana, katika kipengele cha kiongozi bora barani Afrika.

Msigwa amesema mpaka sasa hawana taarifa yeyote juu ya tuzo hizo, na kumekuwa na taarifa zinazosambaa mtandaoni zikionesha cheti ambacho kinadai kuwa ni tuzo aliyopewa Rais nchini Ghana ya kiongozi bora barani Afrika.

“Hatuna taarifa ya tuzo hiyo, tunavyojua ni kwamba mtu yeyote anayepewa tuzo lazima apewe taarifa rasmi kutoka kwa watoaji, sasa hatujapata taarifa yoyote mpaka sasa, nasikia ndio tuzo ambazo kina Monalisa wameshinda, lakini hatujapokea taarifa rasmi kuhusu tuzo hiyo, hivyo siwezi nikaizungumzia”, amesema Msigwa.

Tuzo hizo zimetolewa Aprili 14, 2018 jijini Accra nchini Ghana, ambapo katika tasnia ya filamu nchini msanii Yvone Chery maarufu kama Monalisa amejishindia tuzo ya msanii bora wa kike barani Afrika, Huku Vincent Kigozi maarufu kama Ray akiwa amejishindia msanii bora wa kiume barani Afrika.

Na mwingine ni mpiga picha Moiz Hussein ambaye ameshinda tuzo ya mpiga picha bora barani Afrika kwa mwaka 2017.

Comey amponda Trump, adai hana sifa ya kuwa rais
RC Makonda asitisha wanafunzi kwenda shule, TMA yatoa utabiri

Comments

comments