Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa amemtaka Mbunge na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma kuacha kulalamika na atulie ili polisi wafanye kazi yao.

Ameyasema hayo mara baada ya Mbunge Joseph Kasheku Musukuma kumlalamikia RPC wa Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo kuwa ana roho mbaya na hakutumia busara kumkamata.

Amesema kuwa Musukuma anapaswa kutulia na kukaa kimya ili jeshi la polisi lifanye kazi yake kwani yeye ni mwananchi kama walivyo wengine wanaochukuliwa hatua hivyo hatakiwi kulalamika.

“Msukuma povu la nini, waache polisi wafanye kazi yao, kwani wewe ni mwananchi kama wengine, hivyo punguza kulalamika,acha haki itendeke,”amesema Msigwa

Hata hivyo, Musukuma alikamatwa na jeshi la polisi mkoani Geita na kulala rumande kwa muda wa masaa 24 kwa kosa la kuhamasisha maandamano yaliyopelekea kufungwa kwa barabara inayoelekea katika mgodi wa GGM.

 

Video: Tyga avunja ukimya, aibuka na 'My Way'
Mourinho akoshwa na kiwango cha Matrial