Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa ametupa jiwe gizani kwa wapinzani wao wa kisiasa kwamba wamewashinda kwa hoja zote za kisiasa na wameshindwa kuzijibu hivyo anawashangaa kushangilia ushindi.

Msigwa amesema kwamba wapinzani wao lazima watawashinda kama watatumia vyombo vya usalama na siyo kwa hoja na kwamba wao Chadema wakitoa hoja wao wamekuwa wakishindwa kuzijibu.

Msigwa kupitia ukurasa wake wa Twiter ameandika kwamba “Hatuna mafunzo ya kipolisi wala kijeshi! Mkitumia vyombo vya usalama lazima mtatushinda , lakini tumewashinda HOJA zote za kisiasa! Mmeshindwa kuzijibu! Eti unashangilia Ushindi! Huu ni uporaji” ameandika Msigwa.

Chama cha upinzani CHADEMA kimekuwa kikilalamikia chama tawala kutumia vyombo vya dola katika kuwakandamiza.

Mmiliki wa shule mbaroni kwa kumuua Mwanafunzi
Benki ya Exim yatoa msaada hospitali ya Dodoma

Comments

comments