Naibu Spika, Dk Tulia Ackson Mwansasu amemkabidhi Mbunge wa Iringa  Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili akatoe ushahidi wake wa namna ufisadi ulivyofanyika kwenye mradi wa pasipoti za kusafiria za kielektroniki.

Tulia Ackson amesema hayo baada ya Msigwa kudai kuwa ana taarifa za kutosha juu ya ufisadi uliofanyika katika mradi uliozinduliwa na Rais Magufuli hivi karibuni na kudai kuwa Kambi ya Upinzani bungeni wanazo nyaraka za kutosha ambazo hazina mashaka kuhusu namna ufisadi ulivyofanyika katika mradi huo chini ya Serikali ambayo inajipambanua kupambana na ufisadi.

Kufuatia kauli hiyo Naibu Spika amemuagiza mbunge huyo kwenda kutoa taarifa hizo kwa Kamati ya maadili.

“Mhe. Msigwa taarifa ulizonazo kuhusu ufisadi uliofanyika kwenye hili zoezi zipelekwe kwenye hii kamati, Kamati itakuja kulishauri bunge tufanye nini na huo ufisadi unaoendelea hayo maeneo kwa hiyo naiagiza kamati imuite Mhe. Peter Msigwa na yeye namuagiza Mhe. Msigwa apeleke huko hizo nyaraka ili bunge liweze kushauriwa na kuchukua hatua mahususi” amesema Tulia Ackson.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli  Januari 31, 2018  alizindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 10, 2018
Sugu na mwenzie waachiwa kwa dhamana

Comments

comments