Serikali imesema, bado ipo kwenye mchakato wa kufikisha Bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya habari, ili kuwa sheria kamili, huku wadau wakisubiri tukio hilo kwa shauku kubwa.

Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema bado hatua za maboresho ya sheria ya habari zinaendelea, na kwamba mchakato huo umefika hatua nzuri na unatarajiwa kufanyia kazi, kama ilivyopangwa.

Amesema, “Mchakato umefika hatua nzuri, tutatoa taarifa nini kinaendelea,” amesema Msigwa akijibu swali la wmanahabari lililohoji hatua iliyofikiwa kuhusu mabaoreshio ya sheria hiyo.”

Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa.

Awali, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alipotafutwa kwa lengo la kutoa ufafanuzi, alisema ni vyema akatafutwa au kuwasiliana na Msemaji wa Serikali (Grson Msigwa), ili atoe ufafanuzi wa kina.

Hata hivyo, Tayari serikali imeeleza kupeleka mapendekezo ya sheria ya kulinda taarifa binafsi kwenye bunge linaloendelea sasa, huku maboresho ya sheria ya habari yakiwa kimya.

Wadau wa habari, wanalalamikia sheria mbalimbali za Habari ikiwemo ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, Makosa ya Mtandao 2015, Haki ya Kupata Taarifa ya 2016, Takwimu ya 2015, iliyofanyiwa marekebisho 2019 na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.

STAMICO na GST kutafiti madini Kilombero na Mufindi
Bungeni: Serikali yatangaza kufuta tozo