Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa Chadema na wenzake 12 wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa kwa tuhuma za kuchoma nyumba ya Katibu wa UVCCM mkoani humo na kubomoa nyumba ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwangata aliyehamia CCM, Angelus Lijuja.

Viongozi hao wameshitakiwa kwa makosa makubwa mawili ambayo ni Kula njama na kutenda kosa la kuleta madhara kwenye mali, pia wameshitakiwa kwa uharibifu wa mali uliotokea  Kati ya tarehe 15/1/2018 ambapo waliharibu nyumba ya Anjelus Lijuja yenye thamani ya million saba.

Viongozi waliofikishwa Mahakamani ni pamoja na Peter Msigwa, Leonce Marto, Samwel Nyanda, Adrey George Mkemwa, Rehema Mbetwa, Maneno Rashid Mbuma, Rody Jumanne Makimwa,  Deogratius Faustine Kisumi, Patrick Madat, Luioniso Kadaga na Gama Msigwa

Aidha mwendesha mashtaka amependekeza na kuiomba mahakama kwamba washtakiwa wasipewe dhamana kwa kulinda usalama wao. Wabakie ndani hadi hapo upelelezi utakapokua umekamilika. (sect. 48 mwenendo wa dhamana).

Makonda awaweka mtegoni wafanyabiashara wa magari Dar
Video: Msanii wa muziki apata ajali mbaya