Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amesema kuwa uchaguzi ujao wa mwaka 2020 anaamini kuwa chama chake kitakwenda kushinda kwa kishindo kikubwa.

Amesema kuwa CHADEMA imejipanga na ushindani wa mwaka 2020 katika uchaguzi mkuu ambapo amesema kuwa imani yake ni kuchukua dola.

Aidha, amesema wananchi wameona ni kwa kiasi gani walivyodanganywa na namna ahadi nyingi zilizotolewa zimeshindwa kutekelezwa hivyo anaamini kwamba hawataweza kufanya kosa la kuirudisha CCM madarakani.

“Ushindi wa Chadema 2020 utakuwa ni wa kishindo sana. Wnanchi wamejionea kila mahali wanalia maisha magumu, yamekuwa ni mwiba kwao, na ushindi wetu utakuwa na kasi ya kimbunga,”amesema Msigwa

Hata hivyo, akizungumzia kuhusu suala la yeye kufikiria kuwa Rais siku moja kupitia chama chake, amesema kuwa bado hajapata maono hayo.

 

Willian awapagawisha FC Barcelona, Paulinho afanywa chambo
Riyad Mahrez kuweka rekodi Leicester City

Comments

comments