Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Septemba 12, 2021 amesema kuwa zaidi ya watanania 345, 000 wamepata chanjo ya Uviko- 19, amesema serikali itaendelea kutoa elimu na kuwahamasisha watanzania kuchukua tahadhari tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Serikali katika sekta mbalimbali

“Kampeni kubwa inayofanyika sasa ni kupeleka chanjo vijijini ili Watanzania wengi waweze kuipata. Mwishoni mwa Septemba au mwanzoni mwa Oktoba 2021 tutakuwa na “Wiki ya Uchanjaji” ambapo viongozi wetu wa nchi nzima watapata chanjo” amesema Msigwa

“Hali ya uzalishaji wa umeme kwenye nchi yetu ni nzuri, tunaendelea kuzalisha zaidi ya Megawati 1,600, mahitaji yetu ni Megawati 1,200 na tuna ziada ya Megawati 400”. amesema Msigwa

“Kuna sehemu chache nchini yetu ambazo bado hazijafikiwa na Gridi ya Taifa, ikiwemo mkoa wa Kigoma, wiki iliyopita wananchi wa Kigoma walipata changamoto ya mgao wa umeme, Waziri wa Nishati, Medard Kalemani alikwenda kufanyia kazi changamoto hiyo”.amesema Msigwa

“Kuna baadhi ya maeneo yamepata changamoto ya kukatika kwa umeme, ni kwa sababu ya kazi kubwa inayoendelea ya kubadilisha nguzo zilizooza, na hivi sasa Serikali imeamua kuweka nguzo za zege kwa lengo la kutatua changamoto hiyo” amesema Msigwa

”Serikali moja ya vitu ambavyo inaviangalia ni kuhakikisha tunakuwa na wiki ya uchanjaji. Utaratibu huu sasa unaandaliwa bila shaka mwishoni mwa mwezi wa 9 au mwanzoni mwa mwezi wa 10, tutakuwa na wiki ya uchanjaji” amesema Msigwa

“Tunataka Mtanzania akipata hiyo njia ya mawasiliano katika nyumba yake aweze kupiga simu, kupata intaneti na kutumia televisheni kupitia mtanda” amesema Msigwa

“Hivi karibuni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imekubaliana na TANESCO kwamba itatumia shirika hilo la umeme kusambaza Mkongo wa Taifa” amesema Msigwa

Waziri Bashungwa : Serikali kuendelea kuwainua wasanii
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 12, 2021