Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amewambia wanachama na wafuasi wa chama hicho kuwa wasisubiri kusema ameshinda bila kushiriki zoezi la kupiga kura.

Magufuli amesema hayo leo Agosti 29, 2020   jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

“Tusiridhike tu kwamba Magufuli ameshinda, bali twendeni tukapige kura. Twendeni tukapige kura ili mwaka huu likae fundisho kwa wapingaji wa maendeleo, likawe fundisho kwa wanaotumika na mabeberu na fundisho kwa wasioitakia Tanzania mema,”  amesema Magufuli.

Rais Magufuli anayeomba ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa awamu wa pili, moja ya mambo atakayojinadi katika majukwaa ya kampeni ni pamoja na kupambana na rushwa na kuleta nidhamu serikalini.

CCM imekuwa chama cha pili kuzindua kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu. Jana, Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilikuwa cha kwanza kuzindua kampeni zake.

Bofya hapa kuangalia sehemu ya hotuba ya Dkt. Magufuli:

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 30, 2020
Zlatko awasili Dar, kusaini miwili Young Africans