Kiongozi wa kiislamu, Hamid Slimi (pichani) wa msikiti wa Sayeda Khadija, Mississauga, Canada ameongoza waamini wa dini hiyo wenye nia njema kulifanyia ukarabati kanisa katoliki la Mtakatifu Catherine wa Siena ambalo lilishambuliwa na kuharibiwa na muumini mmoja wa kanisa hilo.

Kwa mujibu wa The Star, Slimi alienda kulitembelea kanisa hilo kuangalia uharibifu uliofanyika ambapo alishtushwa kuona madhabahu yakiwa yameharibiwa vibaya huku Biblia zikiwa zimechanwa hovyo na makaratasi kuzagaa sakafuni.

Kiongozi huyo alirudi na kuwahamasisha waumini wake ambao walichanga kiasi cha dola za kimarekani  5,000 (zaidi ya shilingi milioni 10 za Tanzania) na kufanya ukarabati katika kanisa hilo.

Ripoti zinaeleza kuwa mwanaume aliyefanya uharibifu huo aliyefahamika kwa jina la Hessan aliiambia mahakama kuwa alijikuta akifanya tukio hilo kwa kuwa alichukizwa na dini ya Kikristo.

Hata hivyo, baada ya kufanyiwa uchunguzi, polisi waligundua kuwa Hessan alikuwa na tatizo la akili hivyo wakaamua kumfutia mashitaka yaliyokuwa yakimkabili.

Michuano Ya Wimbledon Open, Moto Wazua Taharuki Uwanjani
Rick Ross Afungwa Kifaa Maalum Mguuni Baada Ya Kukwepa Jela