Mkuu wa kitengo cha sheria katika Baraza la Taifa la usimamizi wa Hifadhi na Mazingira (NEMC), Manchale Heche Suguti ameripotiwa kuanguka ghafla ofisini kwake muda mfupi baada ya kutoka mahakama kuu kitengo cha ardhi, alipoenda kusimamia kesi ya kupinga bomoabomoa iliyofunguliwa na wananchi 681 wa bonde la Mkwajuni jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea Jumanne wiki hii majira ya saa 9:30 alasiri, ambapo alikimbizwa katika hospitali mbili tofauti baada ya tatizo hilo kushindwa kubainika kupitia vipimo vya madaktari wa hospitali hizo.

“Baadaye alipelekwa katika Hospitali ya Aga Khan ambako alilazwa kuanzia siku hiyo (Jumanne) na kutolewa leo asubuhi (jana) baada ya kupata nafuu… ila kwa kifupi ni kwamba afya yake imeyumba na hadi sasa madaktari bado wanachunguza kujua ni kitu gani hasa kinachomsumbua,” chanzo kilikaririwa na gazeti la Nipashe.

Akiongea kwa njia ya simu akiwa katika hospitali ya Agha Khan alipolazwa, Suguti alikiri kukutwa na tukio hilo ambalo  alidai hafahamu nini chanzo chake.

“Kwakweli sielewi kilichotokea. Nilipoingia ofisini kwangu baada ya kutoka kwenye kesi ya nyumba za watu wa Kinondoni, ghafla nikahisi kizunguzungu, giza kutanda na mwishowe nikaanguka… sijui kilichotokea baada ya hapo ila fahamu ziliponirudia nikajikuta nikiwa hospitali,” alisema Suguti.

Kilichomkuta Aliyevaa Bomu Feki la Kujitoa Mhanga jijini Paris
Wachezaji Wa Kigeni Wa Yanga Waikosha Azam FC