Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ametoa msimamo wake mara baada ya kamati ya maadili kumtaka asihudhurie vikao kwa kipindi cha mwaka mzima kwa kosa la kushindwa kuthibitisha hoja aliyodai kuwa bunge ni dhaifu.

Lema amesema kuwa pamoja ya kuwa ana amani kubwa hata mara baada ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa kipindi cha mwaka mzima lakini hatonyamaza hata kama adhabu itakuwa maiti.

Kupitia ukurasa wake wa Twiter amesema hayo ambapo ameandika hivi;

‘’Nimesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge mpaka January 2020. Moyo wangu una imani sana, kwani mahusiano yangu na Haki yanaenedelea kuimarika zaidi… sitanyamaza hata kama adhabu itakuwa mauti’’.

Leo Aprili 4, 2019 Lema amesimamishwa rasmi kutohudhuria vikao vya bunge kwa kipindi cha mwaka mzima hali ambayo imepelekea wabunge kususia bunge na kutoka nje ya bunge kufuatia hukumu hiyo.

Aidha amewatakia wabunge kazi njema katika kutimiza wajibu wa majukumu yao.

Ndugai atoa onyo kali kwa waandishi wa habari wa bungeni
Maonesho ya Tafiti UDSM yameanza rasmi