Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amewataka wafuasi wake wasihuzunike na hatua ya yeye kuwekwa rumande kwa madai ya kutopatiwa dhamana bali watumie nafasi hiyo kuombea tume huru ya uchaguzi.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho bara na mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya kusikilizwa rufaa ya kupata au kutopata dhamana kwa viongozi hao wawili.

“Mwenyekiti amesisitiza sana, kutomlilia yeye bali walilie taifa letu kutafuta mabadiliko, kudai tume huru ya uchaguzi, kwa sababu kesi hii msingi wake ni uchaguzi uliosababisha kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina kwa hiyo naomba wajitokeze kwa waingi kesho pale mahakamani,”amesema Mnyika

Aidha, Mnyika amebainisha kuwa chama hicho kupitia mawakili wake kimewasilisha maombi ya kuiomba mahakama kutoa kipaumbele kwa kesi dhdi ya viongozi wake kabla ya mahakama hiyo haijaenda likizo.

Hata hivyo, Mbowe na Matiko wako mahabusu baada ya kufutiwa dhamana kwenye kesi yao ya msingi inayowakabili juu ya kusababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwilini ambapo walifutiwa dhamana hiyo kwa madai ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

JPM amjulia hali Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
Serikali yatangaza neema ya dawa hospitalini