Mwanamuziki Chris Brown, ameendelea kuonyesha kutoridhishwa na kundi la mashabiki pamoja na wadau wanaolinganisha umahiri wake kwenye tasnia na ule wa nguli wa Pop Hayati, Michael Jackson huku wengine wakimtaja kama msanii bora zaidi yake.

Kufuatia kukithiri kwa aina hiyo ya maoni ya watu juu ya kumlinganisha Chris Brown na Michael Jackson, mwanamuziki huyo ameamua kuvunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa hapendezwi na aina hiyo ya maoni kutoka kwa mashabiki na wadau mbali mbali.

Breezy amesema maoni hayo ni sawa na upuuzi, likiwa ni jibu baada ya kuulizwa ni kwa namna gani huwa nachukulia suala hilo wakati akiwa kwenye mahojiano maalum na Big Boy Tv.

“Huwa najiweka mbali na mada hiyo, Maoni yangu kwenye hilo huwa ni kwamba nisingeweza hata kupumua au hata kuwa na uwezo wa kuimba kama huyu jamaa ‘Michael Jackson’ asingetokea duniani, yuko mbali sana, hakuna ushindani na yeye.” amesema Chris brown.

Wafanyakazi sekta ya Afya waandamana
Wakamatwa kwa kuhatarisha afya za walaji