Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Mshindo Mbette Msolla amewakingia kifua wadhamini wa klabu hiyo kampuni ya GSM, ambao wanatajwa kuwa sehemu ya tatizo linaloendelea ndani ya klabu hiyo kongwe hapa nchini.

GSM wametajwa kuwa chanzo cha tatizo ndani ya Young Africans, wakidaiwa kuingilia majukum ya utendaji wa klabu hiyo, huku wakisahau jukumu la udhamini ambalo lipo kwa mujibu wa mkataba.

Msolla ambaye anapigwa vita na baadhi ya wanachama na mashabiki wa Young Africans kufuatia mwenendo wa timu, amesema suala la kampuni ya GSM kuingizwa kwenye tatizo linaloendelea hivi sasa, sio sahihi zaidi ya wanayanga kuhimizana umoja na mshikamano.

Msolla ameweka wazi kwamba ndani ya Young Africans kila mmoja anatimiza wajibu wake kwa kufanya kile ambacho kinamhusu bila ya kuingiliana katika madaraka.

“Kila mmoja anafanya kazi yake, ikiwa kuna shabiki ambaye hataki GSM kuwa ndani ya Yanga huyo atakuwa sio mwenzetu kwa sababu hatambui yale ambayo wadhamini wetu wanafanya.”

“Kwetu sisi sio wadhamini pekee bali wamekuwa ni patna katika kazi zetu na kila mmoja anatimiza majukumu yake kwa wakati.”

“Mazingira ambayo tulianza nayo awali yanajulikana ila kupitia hawa GSM wameweza kulipa kambi ambayo timu imekuwa ikiweka, tulianza nao pale Legency alilipa miezi sita na kwa sasa tupo Avic ni mwaka mzima amelipa,” Amesema Msolla.

Chini ya Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji Kampuni ya GSM, Young Africans imeweza kuhama kambi kutoka Legency na sasa ipo Kigamboni ambapo inaendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Gomez: Prisons itatusaidia kuipa presha Young Africans
PICHA: Stars yaendelea kujifua Dar