Zoezi la kuboresha huduma za Mawasiliano katika makazi mapya ya wafugaji jamii ya Kimasai litawafanya waweze kupata taarifa mbalimbali Duniani kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa upatikanaji wa huduma za Mawasiliano pamoja na maendeleo ya zoezi la ukusanyaji wa taarifa za Watu na Makazi katika kijiji cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni Mkoani.

“mtakuwa na uwezo wa kuangalia Dunia kutokea Msomera hapa, na sisi kazi yeti ni kuwaunganisheni na Dunia ili mpate hizo huduma na ndiyo maana tumekuja na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), tunataka watoto wenu waanze kujua kuchezea Kompyuta, wajue Dunia inavyoeenda na nina uhakika vijiji vingine vitawaonea wivu Msomera” Waziri Nape

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akifurahia jambo na mmoja wa Wanakijiji wa eneo la Msomera.

Amesema Utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi ni jambo endelevu na hivyo ameongozana na wataalam wa Wizara yake ili kuhakikisha Msomera inawekewa mfumo huo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma nyingine za kijamii na kuifanya Msomera kuwa Kijiji cha Kidijitali.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe ameipongeza juhudi za kufanikisha upatikanaji wa Mawasiliano katika kijiji hicho, ambapo awali kulikuwa na shida ya mawasiliano.

Awali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Msomera, Martin Olykei Paraketi amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha Msomera inakuwa na Mawasiliano bora pamoja na huduma nyingine za kijamii.

Mnara wa masiliano ya simu ukiwa umesimikwa katika Kijiji cha Msomera kilichopo Wilayani Handeni Mkoani Tanga, ili kuwarahisishia mawasiliano wakazi wanaohamia eneo kwa hiari hilo kutoka Ngorongoro.

Jamii ya Wamasai imekuwa ikihamasishwa kuhama kwa hiari kutoka Ngorongoro na kwenda Kijiji cha Msomera cha Wilayani Handeni Mkoani Tanga, kutokana na ongezeko la watu na mifungo inayohatarisha uharibifu mazingira ya hifadhi ya Loliondo.

Ndayishimiye 'ayananga' mataifa ya Ulaya
Serikali yataka huduma bora kwa wananchi