Kijana mmoja kutoka Kinoo, kaunti ya Kiambu, nchini Kenya aliejulikana kwa jina la Moses ameelezea masikitiko yake na kujuta siku aliyomwalika mwanamke aliyekutana naye kwenye mtandao wa Instagram nyumbani kwake.

Kijana Moses mwenye umri wa miaka 30, alihitimu Shahada ya Biashara (B.Com), alikutana na mrembo wake huyo kwenye mtandao wa Instagram mnamo Desemba 10, 2021, na papo hapo akazama ndani ya penzi naye.

“Yule dada alinimaliza na urembo wake. Alikuwa na umbo la kumtoa nyoka pangoni, mweupe na alielewa sana maswala ya fasheni,”

Moses, ambaye huuza viatu katika duka moja karibu na Odeon Cinema, alisema siku tatu baada ya kukutana na mrembo huyo alimuazima KSh 2k sawa na shilingi elfu 40 za kitanzania na akamtumia, bila kufikiria mara mbili.

“Siku sita baada ya kukutana kwenye Instagram, nilimwalika aje kulala kwangu naye akakubali. Nilimchukua mjini mwendo wa saa tisa alasiri na tukaenda K1 Club kufurahia kwa reggae na saa nne baadaye tulienda nyumbani kwangu,” alikumbuka.

Mwathiriwa alisema walikuwa na wakati mzuri na asubuhi ilipowadia mrembo alijaribu kuamka akalemewa na usingizi naye akamwacha akilala akaahidi atarejea nyumbani mapema.

“Nilitaka tuondoke nyumbani pamoja Ijumaa asubuhi lakini alikuwa na usingizi. Nilimwachia KSh 100 sawa na 2033 Tshs mezani ili anunue kifungua kinywa,” alisimulia.

Moses alisema majira ya saa nne asubuhi, Pretty alimpigia simu kumwarifu kuwa ameamka na kumuuliza kama ana nguo chafu ili amfulie. “Nilifurahishwa aliposema alitaka kunisafisha nguo zangu. Nilimwelekeza nilikokuwa nimeziweka na pia nikaahidi kumtumia kuku kutoka KFC ili ale mchana anapoendelea kufua,”

Mchuuzi huyo wa viatu alisema alimpigia simu tena saa kumi jioni na kumtaarifu kuwa anatoka kazini huku akimuomba amwandalia chai naye akakubali. Lakini dakika 40 baadaye, baada ya kufika nyumbani kwake, simu ya Pretty ilikuwa imezimwa na mlango wake haukuwa umefungwa. Alisema alijaribu kumtafuta mrembo huyo kupitia Instagram lakini hakufanikiwa.

“Hela hizo zilikuwa kodi na hadi sasa sijalipa nyumba ambapo huwa inanigharimu KSh 15K kwa mwezi. Sikusherehekea Krismasi kwa sababu sikuwa na raha kwani pesa zangu zilikuwa zimeibwa,” alifichua.

Moses alisema alijiona mjinga kwa kumwamini mtu asiyemfahamu ambaye alikutana naye mtandaoni, na kuwaambia wanaume wawe waangalifu mno wasije wakaangukiwa na masosholaiti wa Nairobi.

Mtibwa Sugar yaivuta Simba SC Manungu Complex
Vivier Bahati achukua gwanda Biashara Utd