Timu ya watoto ya Mgusu Machinjioni imefanikiwa kutwaa taji la GGML- Toto Cup baada ya kuifunga timu ya Elimu Uwangani kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Nyakabale wilayani Geita mkoani Geita katika mashindano mashindano ya soka yanayofanyika kwa kushirikisha watoto wanaozunguka migodi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Ltd (GGML).

GGML ambao ndio waanzilishi na waandaaji wa mashindano hayo, walizindua michuano hiyo katika kata za Mtakuja na Nyankumbu za Geita Mjini kwa lengo la kutoa elimu kwa watoto, walezi na wazazi kuhusu madhara ya kuwanyonya watoto wadogo katika shughuli za uchimbaji madini na kuwanyima fursa ya masomo.

Akizungumza katika fainali hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Terry Strong alielezea furaha yake kwa kuhudhuria katika kilele cha mashindano hayo ya kandanda kwa vijana kutoka eneo jirani la mgodi na kusema tangu kuanza kwa shughuli zao mkoani Geita, uvamizi wa watoto wadogo umekuwa ni changamoto kubwa kwenye eneo la mgodi.

Timu ya watoto ya Mgusu Machinjioni wakifurahia ushindi baada ya kutwaa taji la GGML- Toto Cup kwa kuifunga timu ya Elimu Uwangani kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Nyakabale wilayani Geita mkoani Geita. Waliosimama nyuma ni baadhi ya viongozi wa GGML wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Terry Strong.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa watoto ni sehemu muhimu ya jamii inayozunguka mgodi huo katika kutekeleza shughuli zao za kibiashara na kuongeza kuwa, “Kama sehemu ya kujitolea kwetu kwa jamii, tumefanya uwekezaji mkubwa katika shule, hospitali na kuchangia vifaa mbalimbali vya kutoa huduma. Mathalani mwaka 2018, GGML ilijenga zaidi ya madarasa 600.”

Amesema, “Hii yote ni katika kuwajengea mazingira mazuri ya elimu kwa watoto wetu kwani watoto ni kizazi cha siku zijazo na ndio wanufaika wa kwanza jitihada zote tunazozifanya katika kujitolea kwetu na tunazingatia Kanuni Elekezi za Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Haki za Kibinadamu na Kanuni za Hiari za Usalama na Haki za Kibinadamu (VPSHR) (UNGP).”

Aidha, kwa mujibu wa Strong, idadi ya watoto wanaovamia na kuingia kwenye eneo la mgodi ni jambo ambalo linachukuwa kwa tahadhari kubwa na mgodi huo na kufafanua kuwa, “Kwa kawaida sisi hutumia neno “kuwaokoa watoto” badala ya “wavamizi” kwa sababu watoto wanalindwa na sheria za kitaifa na kimataifa na kati ya mwaka 2019 na 2020, watoto 680 waliokolewa ndani na nje ya eneo la uendeshaji la GGML.

Aidha, ameongeza kuwa, ili kukabiliana na hali hiyo, GGML imeshirikiana na serikali za mitaa kuanzisha programu kadhaa za uhamasishaji, na kusema “watoto tutawafanya kuwa wachangamfu, washiriki program mbalimbali wakati wa mapumziko ya likizo na kukuza hamasa ya kuwa na afya njema, tumechagua kufadhili mashindano ya kandanda kwa ajili ya vijana waliopo ndani na nje ya eneo la mgodi.”

Wanajeshi wa Kenya 'wajipanga' kuwakabili M23
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 2, 2022    Â