Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku ‘Msukuma’ amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania.

Msukuma amechukua fomu hiyo leo Jumanne Januari 11, 2022 katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inakuja baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Job Ngugai kujiuzulu Januari 6 mwaka huu.Uchukuaji fomu kwa Chama hicho ulianza jana Jumatatu ambapo mwisho wa kurejesha fomu hizo ni Jumamosi.

Jana wakati akitoa taarifa ya waliochukua fomu, Msaidizi Mkuu Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Solomon Itunda alisema mpaka jana jioni wanachama tisa walikuwa wameshachukua fomu.

Alisema kuwa upande wa Ofisi ya chama Dodoma waliojitokeza ni pamoja na; Dk Simon Ngatunga, Tumsifu Mwasamale, Merkion Ndofi, Dk Tulia Ackson, Godwin Kunambi na Abwene kajula.

Wengine ni Patrick Lubano, Stephen Masele na Hamidu Chamani kutoka ofisi ndogo Dar es salaam ambapo kwa upande wa Zanzibar hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu

Aliyefunikwa na maporomoko ya mgodi siku 3 apatikana hai
Dogo aliyesaidiwa na Wizkid aingia chaka