Mbunge wa Geita Vijijini Dkt.Joseph Kasheku Msukuma, amesema mfumuko wa bei unaitesa sana Tanzania kutokana na bidhaa mbalimbali kuuzwa kwa bei ghari ukiwemo mchele.

Dkt.Msukuma ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.

Amesema ni vyema Serikali iliangalie suala hilo kwa jicho la tatu ili wananchi waweze kupata unafuu wa maisha kwakununua vyakula kwa bei nafuu.

Mbunge wa Geita Vijijini Dkt.Joseph Kasheku Msukuma

Aidha Msukuma, ameiomba Serikali ihamishe Shule ya Msingi Sahara iliyopo Wilaya ya Nyamagana ili wajenge machinga Complex ambayo itawaweka Wafanyabiashara hao pamoja hatua itakayosaidia kuondokana na changamoto ya kwenda nje ya mji ambayo inapelekea kufilisika kwa mitaji yao.

Wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye Maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza 

“Hakuna kitu kinaniumiza kichwa kama kuwaondoa wamachinga mjini suala la machinga limekuwa gumu hapa Mwanza ndio maana nimeamua kutoa mawazo yangu kwa kumuomba Rais wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu kutenga eneo hilo la Shule ili machinga waweze kufanya biashara zao katika maeneo ya mjini”, amesema Dkt.Msukuma

Panga pangua ya Rais kwa mashirika ya Serikali
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 5, 2023