Kiungo wa Yanga, Simon Msuva amefanikiwa kwa mara nyingine kuwa mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kufikisha mabao 14 yaliyosaidia kwa kiasi kikubwa timu yake kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.

Msuva ni miongoni mwa wachezaji waliocheza kwa kujituma zaidi msimu huu amefanikiwa kuwakimbia wenzake waliokuwa wakimfukuzia kwa karibu nafasi hiyo ambao ni Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting aliyebaki na mabao 13. wengine ni Shiza Kichuya wa Simba, Obrey Chirwa wa Yanga na Mbaraka Yusuph ambao wote wamebaki na mabao 12.

Yanga imemaliza ligi ikiwa na mabao 43 ambayo ni tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakati Simba ikiwa na mabao 33 kama tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, na hivyo kuipiku Simba kwa jumla ya mabao 10 ya kufunga.

Hata hivyo, hii ni mara ya pili kwa kiungo huyo machachari wa pembeni kuibuka kinara wa ufungaji katika ligi hiyo, ambapo katika msimu wa 2014/15 aliibuka pia mfungaji bora.

P- Funk Amfungukia Afande Sele, Amshauri Kumsaidia Harmorapa
Wakulima wa karafuu kunufaika na mkopo