Klabu ya Yanga inajiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayoanza mapema mwakani huku mmoja wa wapinzani wake katika kusaka taji hilo ni mshambuliaji wake wa zamani, Simon Msuva anayecheza Difaa El Jadidi ya Morocco.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linataraji kupanga ratiba ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika keshokutwa Jumatano (Desemba 13) jijini Cairo, Misri.

Michuano hiyo itakayonza mwanzoni mwa Februari na kumalizi Novemba mwakani bingwa atajinyakulia dola 2.5 milioni.

Yanga chini ya kocha, George Lwandamina imedhamiria kufanya vizuri katika michuano hiyo na tayari imeanza kufanya usajili wachezaji mbalimbali wa kimataifa ili kutimiza lengo hilo.

Mabingwa hao wa Tanzania Bara, Yanga itaanza Ligi ya Mabingwa hatua ya awali kama ilivyokuwa kwa Difaa El Jadidi inayoshiriki mashindano hayo kwa mara kwanza tangu 2010 ilipotolewa katika raundi ya kwanza.

Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani hatua ya makundi itashirikisha timu 16, zitakazogawanywa katika makundi manne, kutokana na mabadilino hayo Yanga inaweza kupata nafasi ya kucheza dhidi ya Msuva katika hatua ya awali, au raundi ya pili kama siyo hatua ya makundi.

Msuva amekuwa katika kiwango kizuri tangu Julai 28, 2017, alipotua Difaa El Jadidi akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 15 katika mechi zote.  Msuva amefunga mabao tisa katika mechi 13 za kirafiki, mabao mawili katika Kombe la Mfalme katika Ligi Kuu Morocco ‘Batola Pro’ amefunga mabao 4, katika mechi 10.

Akizungumzia ratiba hiyo Msuva alisema sitamani tupangwe dhidi ya Yanga hata kidogo, lakini ikitokea hivyo nitawajibika kuipigania Difaa.

“Ukweli ni kwamba Yanga ni timu yangu, imenilea mpaka kufikia hatua ya kuhitajika na timu kadhaa kubwa barani Afrika, lakini Difaa nipo ni kazi si kingine.

“Pamoja na huku, lakini nimekuwa nikiwasiliana mara kwa mara na wachezaji wa Yanga, hii inaonyesha namna gani ambavyo bado ni kama nipo Yanga vile, ndiyo maana nikatangulia kusema sitamani tupangwe pamoja.

“Ila yote kwa yote ya uwanjani yatabaki”.

Rais Kenyatta ampa pole JPM
Waliofuzu nane bora ligi ya wanawake hawa hapa