Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) wamekutana na kuzungumzia miswada sita iliyowasilishwa katika Bunge lililomalizika huku wakionekana kufurahia zaidi mswada wa Sheria mpya ya vyama vya siasa.

Akizungumza jijini Dodoma, Katibu wa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jason Rwekiza amesema kuwa wamelazimika kuzungumza na waandishi wa Habari ili wananchi wapate kile ambacho kimefanyika Bungeni kupitia Bunge hilo.

Amesema kuwa moja ya miswada ambayo imepitishwa na Bunge ni pamoja na miswada wa Wakala wa maji vijijini ambao wamefanikiwa kuupitisha kwa maslahi mapana ya wananchi.

Akizungumzia kwa kirefu kuhusu mswada wa Sheria ya vyama vya siasa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda amesema kuwa mswada huo ni muhimu sana kwani vyama vinaondokana kuwa vyama vya mfukoni na kuwa Taasisi.

Aidha, Mapunda amesema kuwa Sheria hiyo imetoa Heshima ya kuheshimu uwepo wa mapinduzi ya Zanzibar na pia Sheria imeleekeza nyaraka zote za vikao na maamuzi yake kutunzwa kwa msajili wa vyama vya siasa ambaye kimsingi ndio mlezi.

Kwa upande wake Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi amesema kuwa yamefanyika marekebisho mbalimbali ya Sheria ikiwa pamoja na Kupandishwa hadhi kwa hifadhi na kuwa Hifadhi za taifa ambapo Tanapa wataweza kujenga Hotel na mambo mengine ya kitalii, huku akizitaja baadhi Hifadhi hizo kuwa ni Hifadhi ya Biharamulo, Rumanyika, na zinginezo ambazo kwa ujumla wake zitaleta tija kwa taifa na kutoa wito kwa Tanapa kuwekeza katika maeneo hayo.

Hata hivyo, wabunge hao akiwamo Alani Kiula wa Iramba Mashariki, walitolea ufafanuzi juu ya malalamiko ya madai ya kupotea kwa Fedha shilingi tirioni 1.5 na zinginezo na kusisitiza kuwa hakuna Fedha iliyopotea kwa mujibu wa taarifa ya CAG aliyowasilisha Bungeni

 

Wizara ya Kilimo kuja na Sheria ya kumtetea Mkulima
Mkuu wa Majeshi ateta na Kamati ya Ulinzi na Usalama Njombe