Moto mkubwa uliozuka usiku wa kuamkia leo jijini Nairobi nchini Kenya umeteketeza makazi ya watu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa Kijiji eneo la Langata nchini humo.

Moto huo uliozuka majira ya saa mbili usiku na kuenea kwa haraka zaidi chanzo chake bado hakijajulikana, ingawa Magari manne ya Jeshi la zima moto yalijaribu kuuzima lakini hayakweza kuufikia kutokana na njia kuwa nyembamba mtaani hapo.

Aidha, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Taifa ya Kukabiliana na Majanga anayeshughulikia mawasiliano, Pius Masai ameliambia Gazeti la Nation kwamba walilazimika kuomba msaada zaidi wa magari ya zima moto lakini maafisa walichelewa kufika eneo la tukio.

Hata hivyo, Moto huo baadaye ulizimwa, ingawa moshi bado ulikuwa unafuka katika baadhi ya maeneo asubuhi, huku wananchi wakisema wamepoteza mali zao nyingi.

Arsenal yakaribia kumnasa Aubameyang
Video: Polepole avunja ukimya Lissu kupigwa risasi, Rafu za uchaguzi zaanza Kinondoni