Uongozi wa klabu ya Young Africans ipo mbioni kukamilisha mpango wa ajira ya kocha mpya ambaye atachukua nafasi ya Luc Eymael aliyefungashiwa virago siku moja baada ya kumalizika kwa msimu wa 2019/20, kwa mabingwa hao wa kihistoria Tanzania Bara kuichakaza Lipuli FC bao moja kwa sifuri pale Iringa na kushusha daraja.

Viongozi wa Young Africans wamekua wakipokea maombi ya kazi kutoka kwa makocha wa kimataifa na wale wazawa, lakini bado imeendelea kuwa siri kwa upande majina yao.

Kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo yenye maskani yake jijini Dar es salaam Simon Patrick alithibitisha kupokea maombi mengi kutoka kwa makocha wazawa na kwingineko duniani.

Lakini pamoja na katibu mkuu kuthibitisha hilo, tetesi zinaeleza kuwa huenda Young Africans ikaangukia kwa kocha wa kitaliano ambaye anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa kupitia wasifu wake.

Watu wa karibu na kocha huyo wamekuwa na mawasilino na Dar24 na kueleza kwa undani, vipi rafiki yao anavyopewa kipaumbele katika harakati za kupata ajira ndani ya Young Africans.

Kocha huyo anaeitwa Giovani Scanu alizaliwa Mei 3 mwaka 1975 katika mji wa Nauro uliopo kwenye kisiwa cha Sardinia magharibi mwa bahari ya Mediterranean.

Kama ni mwanamahesabu mzuri utabaini kocha huyo bado kijana, kwani ana umri wa miaka 45, ana leseni yenye hadhi kubwa inayotambuliwa na shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA Pro Licence), ni dhahir inatosha katika vigezo vya kufanya kazi kwenye Ligi ya Tanzania Bara.

Kocha huyo amewahi kufanya kazi katika nchi kadhaa duniani ikiwepo barani Afrika.

Nchi alizowahi kufanya kazi ni nchini kwao Italia, Brazil, Lithuania, Hungary, Bangladesh, Moldova na Nigeria.

Ufuatao ni wasifu mfupi wa kocha SCANU GIOVANI

TIMUNAFASIDARAJANCHIKUANZA KAZIKUONDOKA
SEF Tempio PausaniaKocha msaidizi3Sardinia, Italia06/07 (Jul 1, 2006)06/07 (Jun 30, 2007)
ComoKocha msaidizi3Sardinia, Italia07/08 (Jul 1, 2007)07/08 (Jun 30, 2008)
AlgheroKocha msaidizi3Sardinia, Italia08/09 (Nov 1, 2008)09/10 (Jun 30, 2010)
SS Tavolara CalcioKocha msaidizi3Italia10/11 (Oct 1, 2010)10/11 (Feb 10, 2011)
Nuorese CalcioKocha mkuu1Sardinia, Italia11/12 (Jul 1, 2011)11/12 (Dec 31, 2011)
FK Tauras TauragėKocha mkuuLigi kuuLithuania11/12 (Jan 1, 2012)12/13 (Dec 30, 2012)
Kaduna United F.C.Kocha mkuuLigi kuuNigeria13/14 (Jul 1, 2013)13/14 (Jun 30, 2014)
FK Tauras TauragėKocha mkuuLigi KuuLithuania14/15 (Jan 1, 2015)14/15 (Jun 30, 2015)
Coritiba FCKocha mkuuLigi daraja la piliBrazil15/16 (Nov 4, 2015)15/16 (Jun 30, 2016)
Tatabánya SCKocha mkuuDaraja la piliHungary16/17 (Nov 30, 2016)16/17 (Jun 30, 2017)
Brothers UnionKocha mkuuLigi kuuBangladesh17/18 (Jul 12, 2017)17/18 (Aug 5, 2017)
FK NevezisKocha msaidiziLigi kuuLithuania17/18 (Jan 1, 2018)17/18 (Jan 31, 2018)
Zimbru ChisinauKocha mkuuLigi kuuMoldova19/20 (Feb 9, 2020)19/20 (Jun 9, 2020)
Tshishimbi: Nitarudi nyumbani DR Congo
Wagonjwa wa Saratani KCMC wapata neema