Mtalii wa Marekani  amekamatwa akiwa na kichwa cha mwanamke kwenye begi lake nchini Japan.

Mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Yevgeniy Bayraktar mwenye umri wa miaka 26 anashikiliwa na jeshi la polisi la Osaka kufuatia tukio hilo.

Picha za CCTV zimemuonesha akiwa na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 27 karibu na kituo cha treni usiku wa manane. Kisha, wawili hao waliingia kwenye nyumba moja aliyofikia mwanaume huyo.

Kwa mujibu wa rafiki wa mwanamke huyo, marehemu alimuaga kuwa anaenda kukutana na mwanaume ambaye walikutana kwenye mitandao ya kijamii na hawakuwahi kuonana ana kwa ana awali.

Tukio hilo lilitokea Februari 16 ambapo siku iliyofuata familia ya mwanamke huyo ilipata wasiwasi na kutoa taarifa polisi baada ya kutomuona ndugu yao akirejea nyumbani tofauti na kawaida yake.

The Telegram imeripoti kuwa Kamera za wanausalama zilimuonesha mwanaume huyo akiingia na kutoka kwenye nyumba hiyo mara kwa mara akiwa na begi lakini hakukuwa na ishara yoyote ya kuwa na mwanamke huyo ambaye awali alionekana naye.

Baada ya kuvamia na kupekuwa walikuta kichwa cha mwanamke huyo kwenye begi lake.

Bayraktar aliingia nchini Japan kwa lengo la kufanya utalii na alikodi sehemu ya nyumba hiyo kwa ajili ya kukaa kwa muda wa wiki moja.

Simba yapangiwa waamuzi wa Afrika Kusini
Yanga kuchezeshwa na waamuzi kutoka Burundi