Mtangazaji Fred Fidelis maarufu kama Fredwaa amefariki dunia leo Juni 12, 2021 baada ya kupata ajali leo Kawe, Dar es salaam.

Fredwaa amewahi kufanya kazi Times FM Dar es salaam, Radio Free Africa Mwanza pamoja na CloudsFM Dar es salaam.

Aliwahi kujulikana sana na kujipatia umaarufu akiwa mtangazaji wa kipindi cha Vodacom Burudani sana alichokuwa akikifanya kupitia Redio Free Africa.

Kituo cha habari cha CloudsFM wamethibitisha taarifa za kifo hicho.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mwananchi Digital, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema chanzo cha ajali hiyo ni ulevi na kwamba wanamshikilia dereva wa gari hilo.

“Inaonekana dereva alikuwa amelewa wakati akiendesha gari liliacha njia na kuingia mtaroni eneo la Tanganyika Packers karibu na sehemu ambayo Mchungaji Boniphace Mwamposa huwa anatoa neno, mtangazaji (Fredwaa) alifariki ila dereva tunamshikilia,” amesema Kingai.

Mmiliki wa Amazon arudi tena kileleni kwa utajiri
Ajira kwa watoto yapindukia