Mtanzania anayedaiwa kuwa mfuasi wa kundi la kigaidi la Al Shabaab la nchini Somalia, ameripotiwa kuhukumiwa kifo katika mahakama ya kundi hilo baada ya kubainika kuwa ni mpelelezi.

Mtanzania huyo aliyetajwa kwa jina la Issa James Mwesiga alifikishwa katika mahakama ya Alshabaab, kusini mwa Somalia ambapo alisomewa mashtaka na mwisho kuelezwa kuwa amekutwa na hatia ya usaliti kabla ya kuamriwa kuuawa kwa kupigwa risasi.

Maafisa wa Alshabaab walieleza kuwa Mwesiga alikuwa akipambana pamoja na wanamgambo wengine wa kundi hilo tangu alipojiunga mwaka 2013 lakini baadae alibadilika na kuwa mpelelezi, ingawa haikutajwa alikuwa anapeleleza kwa maslahi ya nchi gani.

“Mwesiga aliuawa na wanamgambo wa Al Shabaab wakiongozwa na Ahmed Suraq,” mkazi wa eneo ambalo tukio hilo lilifanyika aliliambia Shirika la Habari nchini humo, Somali National News (SONA).

 

Misri Kujiuliza Tena Kwa Serengeti Boys Kesho
PSG Wajipanga Kuvunja Rekodi Ya Usajili Duniani