Kijana wa kitanzania ameshinda tuzo kubwa za ubunifu ‘Inter-continental innovation competition awards’ na kuwashinda waafrika wenzanke na wengine kutoka bara la Ulaya na Asia.

Given Edward mwanzilishi wa kampuni ya Teknolojia ‘Mtabe’ ambayo hutumia mfumo wa ujumbe mfupi (sms) kutoa maudhui ya elimu kwa wanafunzi ambao hawakidhi kununua gharama za vitabu tena bila kutumia mtandao wa (Internet Access).

Mtanzania huyo ameweza kuchukua tuzo mbili (Best Social Innovation from Africa) na (Youth Overall Best Innovation Awards) – shindano hilo limefanyika Graz nchini Austria kuanzia November 28 hadi December 1 ambapo lilikutanisha mamia ya vijana wabunifu (innovators) kutoka pembe zote za dunia,huku Tanzania ikipeperusha vizuri bendera katika masuala ya ubunifu na kuchukua tuzo.

NEC yatoa somo kwa wasimamizi wa uchaguzi
Uwekezaji katika sekta ya madini waongezeka

Comments

comments