Bendera ya Tanzania inaendelea kupeperushwa na watanzania wanaojituma katika ubunifu wa mambo mbalimbali hata kufikia hatua ya kuwashinda watu wa mataifa yaliyoendelea.

Mtanzania, Edward Loure  ambaye ni mmasai asilia anayeishi maisha hayo, amekuwa muafrika pekee aliyetangazwa jana kushinda tuzo ya dunia ya mazingira inayofahamika kama ‘Goldman Environment Prize’, ambayo ni tuzo kubwa zaidi duniani ya shughuli za mazingira.

Loure alitangazwa kuwa mmoja kati ya washindi sita wa tuzo hiyo wa mwaka 2016, waliofanya vizuri katika kazi za utunzaji mazingira na shughuli za kijamii, wakichukuliwa kutoka katika mabara sita wanayoishi binadamu.

Sifa kubwa iliyompa nafasi Loure kwenye tuzo hizo ni uamuzi wake wa kuwasaidia watanzania wanaoishi katika eneo la bonde la ufa kupata hati za viwanja kwa ukubwa wa ardhi yenye ekari 200,000. Upatikanaji huo wa hati za ardhi uliwasaidia watanzania hao kutoharibu mazingira.

Wengine waliopata tuzo ni pamoja na Leng Ouch wa Cambodia, Zuzana Caputova wa Slovakia, Luis Jorge Revra wa Puerto Rico, Destiny Watford wa Marekani na Maxima Acuna wa Peru.

Magufuli akataa Daraja la Kigamboni kuitwa jina lake, ataka liitwe ‘Daraja la Nyerere’
Magufuli kuzindua Daraja la Kigamboni