Klabu ya Tottenham Hotspurs imeendelea na mkakati wa kuwasainisha mikataba mipya baadhi ya wachezaji wake, ikiwa ni sehemu ya kuepuka fitna ambazo huenda zikajitokeza wakati wa usajili wa majira ya baridi (Januari) pamoja na majira ya kiangazi (Juni-Agosti) mwaka 2017.

Muda mchache uliopita ilikua zamu ya beki wa pembeni Danny Rose ambaye amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka White Hart Lane hadi mwaka 2021.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26, anakuwa mchezaji wa saba kukubali kusaini mkataba mpya, akitanguliwa na Dele Alli, Eric Dier, Christian Eriksen, Kevin Wimmer, Tom Carroll pamoja na Harry Winks.

Wachezaji wengine ambao wapo katika hatua za mwisho kabla ya kusaini mikataba mipya ya kuendelea kuitumikia Spus ni Kyle Walker pamoja na Jan Vertonghen.

Rose amejihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza chini ya utawala wa meneja Mauricio Pochettino na mwishoni mwa msimu uliopita alitajwa katika kikosi bora cha ligi kuu ya soka nchini Uingereza (PFA Premier League Team of the Year).

Alianza kuwika na kutambuliwa na mashabiki wa soka duniani, kufuatia bao zuri alilofunga wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England msimu wa 2010/11 ambapo Spurs walicheza dhidi ya mahasimu wao wa kaskazini mwa jijini London Arsenal.

Aliko Dangote: Nitaimiliki Arsenal Ndani Ya Miaka 3-4 Ijayo
Luis Enrique: Kuumia Kwa Lionel Messi Ni Pigo La Dunia