Kiungo wa zamani wa klabu ya Simba SC Mtemi Ramadhani, ametoa tahadhari kwa benchi la ufundi la klabu ya Simba lililopo chini ya kocha mkuu Gomes Da Rosa kuelekea mchezo wao wa na Al Ahly February 23, 2021 jijini Dar es Salaam.

Mtemi amemtaka Gomes kujipanga vyema kuimaliza mechi hiyo hapa nyumbani kwakuwa haoni kama Simba anaweza kupata matokeo mazuri nchini Misri.

“Ni mechi ngumu sana kutokana na ubora wa Al Ahly kwa sasa. Ni lazima kocha ajipange vyema kuchukua alama tatu hapa nyumbani. “ Amesema Mtemi.

Mtemi amegusa masuala ya kiufundi akimtaka kocha huyo kutumia washambuliaji wawili katika mechi ijayo na sio mfumo wa mshambuliaji mmoja ili kuepuka kucheza defensive kitu ambacho kinaweza kuwanyima matokeo mazuri kwa kukosa balansi nzuri ya safu ya ushambuliaji.

“Amekuwa akimtumia Mugalu au Kagere lakini ukiwatazama Al Ahly wamekamilika sana kukulazimisha muda wote kuwa nyuma ya mpira. Kocha ni lazima awe na muunganiko kamili kuanzia eneo la kiungo mpaka safu ya ushambuliaji. Mimi ni muumini wa double striking system kwenye mechi ngumu” Alisema Mtemi.

Mtemi Ramadhani ndio mchezaji mzawa wa kwanza kabla ya Nadir Haroub kuwafunga Al Ahly juu ya ardhi ya Tanzania akifanya hivyo mwaka 1985 Simba iliposhinda 2-1.

Tozo za fukwe zapigwa marufuku
Tanzania, EU zasaini mkataba wa Bil. 307.9